Abdillatif Abdalla

Rate this post
Abdillatif Abdalla alizaliwa mnamo tarehe 14/4/1946 mjini Mombasa katika mtaa wa Kuze. Baada ya kushawishiwa na nduguye Sheikh Abdillahi Nassir  ndipo alipoingia katika siasa. Bwana huyu aliweka historia mwaka wa 1969 ya kuwa mfungwa wa kwanza wa kisiasa baada ya Kenya kupata uhuru wake akiwa na miaka 22 tu. Abdillatif  alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na nusu, lakini baada ya aliekuwa waziri wa sheria wakati huo Charles Njonjo kukata “appeal” mahkama ikaamua kumfunga miaka mitatu kwa kosa la kuandika  makala aloyaita ‘Kenya twendapi?’ na hii ilikuwa nakala ya saba aloiyandika kijana huyu. Humo alishtumu vikali utawala wa Rais mwenda zake Mzee Jomo Kenyatta na waliokuwa kwenye mamlaka wakati huo.
Alipokuwa kifungoni katika gereza la Kamiti aliadhibika si haba , kama asemavyo mwenyewe ni alikuwa katika gereza ndani ya gereza wala hakuwa na ruhusa ya kutoka wala kuwasiliana na mtu yoyote,  na hakuruhusiwa kupewa kalamu wala daftari. katika kulindwa kwake aliekewa askari wawili kwa bahati nzuri mmoja wa askari hao akawa rafiki yake ambae alimpa kalamu licha ya vikwazo aloekewa. Wakati wake mwingi aliutumia kuandika mashairi huko gerezani
Mwaka wa 1972 mkusanyiko wa mashairi yake ulipigwa chapa na kutolewa kitabu kilopewa jina ‘sauti ya dhiki’ kilicho haririwa na marehemu Shihabudin Chiragdin. Kitabu hiki kilipata bahati kubwa ya (Kenyatta literary award) mwaka wa 1974. Na lugha alioitumiwa Abdilatif ni ile ya kimvita (Kiswahili cha Mombasa) Baada ya hapo aliishi uhamishoni na  kupokewa na rais wa Tanzania mwendazake Julius Nyerere katika chuo kikuu cha Dar es salam ambapo alifanya kazi na taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili kwa miaka kadhaa. Alipotoka Tanzania alienda Uingereza na kufanya kazi na shirika la BBC Swahili service kama mwana habari. Alipokuwa  huko pia aliendelea na harakati zake zinazohusu siasa za Kenya, hata wakati mmoja katika utawala wa Rais Moi alitumiwa watu wawili huko uingereza kutoka Kenya ili wamshawishi awachane na harakati zake na kumuahidi vinono vingi, nae kwa moyo wa ujasiri akakataa kata kata. Hatimae akastaafu alipokuwa nchini Ujerumani kama muhadhiri wa chuo kikuu cha ZMO baada ya kufundisha fasihi ya Kiswahili.
Kwa wanaomfahamu abdilatif abdalla hawatoshangaa sana kwa ufundi wa kuandika mashairi yake, labda hii ni kwa ajili ya mazingira aliyoinukia. Maana amezaliwa katika kitovu cha uswahili katika mtaa wa kuze ambako ni mahali alozaliwa Yule shaha wa malenga wa zamani  Muyaka wa Muhaji. Na kwao mwenyewe kumetokeya washairi akiwemo nduguye Ustadh Ahmad Nassir (Ustadh Bhalo), wasomi, wana siasa kama vile nduguye sheikh Abdillahi Nassir> vile vile pia kumetokea waimabaji kama marehemu Mohamed Khamis Juma Bhalo na hata waimaji na wapiga ala nza kienyeji. Mradi amekulia katika mazingira ya usanii na kisiasa. Hivi sasa Bwana Adillatif anaishi nchini Ujerumani.
Facebook Comments

About author View all posts